Monday , 1st Jun , 2015

Hali ya kiafya ya msanii wa muziki Size 8 wa nchini Kenya, imeripotiwa kuimarika kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kutoka hospitali alipokuwa amelazwa, shida yake kubwa ikielezwa kuwa ni presha ya kupanda.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Size 8

Star huyo pia kwa njia ya mtandao ameweka wazi kuwa ameweza kuendelea na mazoezi kujiandaa na maonesho, kubwa zaidi likiwa ni katika jukwaa kubwa la sherehe za tuzo za Groove ambazo zitafanyika tarehe 6 mwezi huu.

Staa huyo ambaye pia ana ujauzito anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa daktari katika kipindi hiki ili kuenda sawa na kuijali afya yake.