Monday , 3rd Sep , 2018

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Dayna Nyange amesema anajitambua anachokifanya kwenye maisha yake, hivyo haoni hatari yoyote kwa yeye kuzungumziwa vibaya juu ya maisha yake.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Dayna Nyange

Dayna ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na EATV, baada ya kuwepo 'skendo' za mwanadada huyo kwamba anaongoza kuwa na mahusiano mapya kila kukicha bila ya kuhofia jambo lolote.

"Siyo mbaya watu kuniweka katika orodha ya wanawake wenye mahusiano mapya kila kukicha kwasababu kila mmoja anaongea kila anachotaka, ila mimi ndio najua nipo vipi na kitu gani ninachohitaji kwenye maisha yangu",amesema Dayna.

Dayna Nyange ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaoitendea haki tasnia ya muziki nchini, ambapo siku ya Ijumaa iliyopita aliweza kuachia ngoma yake mpya ya salama ndani ya kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE kinachorushwa na EATV.

Mtazame hapa chini Dayna Nyange akifunguka zaidi