Tuesday , 2nd Dec , 2014

Mtayarishaji muziki Sheddy Clever ambaye ndiye anahusika katika kutengeneza project nyingine kubwa kabisa kutoka kwa Diamond, 'Ntampata Wapi' ametoa ya moyoni kuhusiana na ishu ya kutopatiwa utambulisho wa maandishi katika video ya ngoma hiyo kali.

mtayarishaji wa muziki wa bongofleva nchini Sheddy Clever

Sheddy amesema kuwa, ameona utaratibu huu upo katika video kubwa za wasanii wanaofanya vizuri Afrika pia, ingawa haelewi ni kwanini watayarishaji wa ngoma kwa upande wa audio hawapewi mashavu yao.