Saturday , 11th Apr , 2015

Baada ya kuitawala wiki kwa gumzo kutoka picha moja matata ya busu la kifaransa (French Kiss) kati ya Ney wa Mitego na Shamsa Ford, Staa huyo wa filamu aibuka na kummwagia sifa Ney.

Ney wa Mitego na Shamsa Ford

staa huyo wa filamu ambaye alikanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ney, amemmwagia sifa staa huyo wa muziki na kusema kuwa tofauti na wengi wanavyochulia, ni mtu mmoja mpole na mkarimu sana.

Shamsa kupitia mahojiano tuliyofanya naye, amekazia kuwa Ney ni kijana mchakarikaji, anayehamasisha vijana wengine, na sifa nyingine kem kem ikiwepo kauli tata kuwa Ney ni kijana mwenye mapenzi tele.

Itakumbukwa kuwa, wiki hii pia tuliongea na Ney ambaye alituchanganya kabisa na maelezo kuwa Shamsa ni ndugu yake, swali likabaki kuwa picha iliyoonekana ni ya projekti ya video ama movie, na hapo akatuchanganya kuwa picha ile ni scene katika video, ambapo baadaye akabadilika na kusema kuwa ni movie, msilikize mwenyewe hapa.