Monday , 14th Jul , 2014

Msanii wa kike nchini Tanzania Shaa ambaye hivi sasa amefyatua wimbo wake mpya 'Subira' ataungana na wasanii mbalimbali kutoka barani Afrika katika kutengeneza muziki wenye mchanganyiko wa vionjo vya kisasa vyenye asili ya Afrika.

msanii wa kike nchini Shaa

Shaa pamoja na Joh Makini wataungana na wasanii kutoka Afrika Mashariki wakiwemo Fena, Rabbit, Jay A, Victoria Kimani, Navio, Jackie Chandiru na Lillian Mbabazi.

Aidha wasanii kutoka Nigeria Burna Boy, Flavour, Iyanya, Waje na Olamide pia Neyma na Jose Valdemiro kutoka Mozambique watajumuika pamoja kutengeneza nyimbo hizo za kiafrika zitakazofanyika katika studio kubwa inayomilikiwa na kampuni ya vinywaji laini.