Monday , 2nd Mar , 2015

Msanii wa miondoko ya bongofleva nchini mwanadada Saraha ambaye alikuwa nchini Sweden-Stockholm akiandaa kazi zake mpya za muziki hivi sasa ametua nchini Tanzania tayari kwa ajili ya shoo ya project yake mpya iliyobatizwa jina 'Come Together'.

msanii wa bongofleva mwenye makazi yake nchini sweden Saraha

Saraha ameiambia eNewz kuwa atakuwepo nchini kwa muda wa wiki moja katika shoo hiyo maalum kwa ajili ya kusaidia watoto na vijana walemavu nchini.

Aidha, mwanadada huyo amegusia kuwa kuanzia mwezi huu mashabiki wake wakae tayari kuupokea wimbo wake mpya wa kwanza ulioimbwa kwa lugha ya Kiswedish uliochanganywa na style ya bongofleva na house music uliotengenezwa na prodyuza mmoja kutoka nchini Sweden.