Sherehe hizo za utoaji wa tuzo ambazo ni kubwa zaidi Afrika Mashariki na zinafanyika kwa mara ya kwanza , zitatolewa Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam
Baada ya East Africa Television LTD kumtangaza Salama Jabir mwenyewe alionyesha kufurahia na alitumia akaunti yake ya Twiiter kuweka ujumbe maalum wa kuonesha furaha yake
Wadau mbalimbali nao hawakuwa nyuma kuonesha shangwe zao kwa kufurahia habari njema ambayo kwa sasa ndio gumzo la Afrika Mashariki, huku wakiandika hisia zao na kutoa pongezi.