Thursday , 26th Jan , 2017

Msanii wa hip hop Bongo, Roma Mkatoliki amesema muziki wa hip hop una ufundi wake na majingambo yake kwenye kuimba hivyo inaruhusiwa kuimba unachotaka.

Roma Mkatoliki

 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Roma amesema "Huwezi kumzuia msanii kuimba kitu chochote katika nyimbo yake na wengine wanatumia njia za kudiss wasanii wenzao kama njia ya kujionesha kuwa wanauwezo wa kuchana na kuimba vizuri kuliko msanii mwingine wa hip hop".

Pia Roma amesema wengine wanaamua kuwachana na kuwaimba wasanii wakubwa katika wimbo zao ili kutafuta 'kiki' za kuwatoa au kuangalia soko la muziki akiamini kwamba kama atamchana msanii mkubwa watu watamsikiliza na kuanza kufuatilia muziki wake.