Thursday , 12th Feb , 2015

Rapa ROMA Mkatoliki, amewataka vijana kuamka na kujishughulisha hasa katika kusaidia jamii ili kuacha alama na heshima ambayo itawajengea maana nzima ya uwepo wao hapa duniani.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Roma Mkatoliki

Kwa nafasi yake star huyo amesema kuwa, kupitia muziki anaofanya anafurahi kuona kuwa kazi yake inaelimisha, inahamasisha na kumjengea heshima kutoka kwa wale wanaomzunguka, na hata kutoa nafasi za vipato kwa wengine.