Thursday , 20th Mar , 2014

Ikiwa kama ndio kwanza anafungua mwaka huu kimuziki, Msanii wa muziki Black Rhino yupo katika hatua za mwisho kabisa kudondosha ngoma yake mpya kabisa ambayo ameifanya na Marehemu Mangwea, kazi ambayo ameipatia jina “Lookie Lookie”.

Kuhusiana na kazi hii ambayo imefanywa na prodyuza Mbezi, Black Rhino ambaye ana utambulisho wa aina ya kipekee ya flow katika muziki wa Bongo, amefafanua kwa mashabiki wake juu ya kazi hii, ya kolabo na Ngwair na ni kwanini anataka kuiachia wakati huu kupitia mahojiano yake na eNewz hapa.