Wednesday , 11th Mar , 2015

Rama Dee, ambaye ameachia rekodi mpya inayokwenda kwa jina 'Usihofie Wachaga' ametumia nafasi yake kuwaasa wasanii wenzake kutosahau kuambatanisha mafundisho ya aina fulani katika muziki wao kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na cha baadae.

msanii wa R&B nchini Tanzania Rama Dee

Rama Dee mwenye makazi yake huko Australia sasa, amesema hayo akizungumzia muziki wa Tanzania ulipofikia sasa huku akikiri kuwa upo katika hatua nzuri, kukiwa bado na kazi ya kupunguza wasanii wale ambao hawana uwezo na kutoa nafasi kwa vipaji halisi.