Tuesday , 1st Apr , 2014

Wasanii wakubwa wa muziki kutoka nchini Kenya, Prezzo pamoja na Nonini hivi karibuni wameungana na kutumia muda kukaa pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kufurahia burudani mbalimbali pamoja nao katika kituo chao huko Kayole.

Katika tukio hili la aina yake, watoto hawa walipata nafasi ya kufurahi pamoja na mastaa hawa ambao walijiweka katika hali ya kawaida na kujichanganya nao katika michezo mbalimbali.

Kivutio kikubwa katika tukio hili kilikuwa ni mtoko wa Prezzo aliyezoeleka kwa kutupia ming'ao ama bling bling, kutokelezea katika tukio hili akiwa amevaa malapa na kujichanganya kama kawaida na wenyeji wake.