Tuesday , 19th Jan , 2016

Kufuatia msanii wa muziki Linex kupiga picha za Harusi na baadaye kujulikana kuwa lengo la picha hizo ni kwa ajili ya kava la ngoma yake mpya ya 'Kwa Hela', mapya yameibuka baada ya msanii huyo na modo wa kava hilo kuzidisha ukaribu wao kimahaba.

Baada ya kufuatilia kwa karibu, ili kufahamu ukweli wa mambo, eNewz tumeongea na modo wa kava ya rekodi ya Linex - bibi harusi, Erica juu ya kazi aliyofanya na Linex, na aina ya mahusiano aliyonayo sasa, ikionekana kuwepo na hisia za mapenzi kati yao.

Linex pia, naye akalazimika kufafanua jambo, hasa baada ya kuonekana akiwa karibu na mrembo huyo, hata baada ya kazi kuisha, ambapo hapa ananyoosha maelezo.