
Octopizzo pia akaweka wazi kuwa, baada ya muda akiwa na ndoto za upishi, mawazo yake yalihamia katika ndoto za kuwa Polisi akiwa na umri wa miaka 7 tu, ndoto ambayo nayo haikudumu kwa muda mrefu kabla ya kujiwekea lengo kuwa ni lazima afanye kitu ambacho atakiendesha kwa nguvu ili kufika juu, na hapo ndipo safari yake ya muziki ilipoanza.
Rapa huyu amesema haya wakati akitoa ushauri wake kwa wasanii wanaochipukia ambapo amewataka kutengeneza lengo na kulifanyia kazi kwa bidii ili kuweza kutoka.