Friday , 21st Nov , 2014

Safari za staa wa muziki wa rapa Kenya, Octopizzo kujitangaza katikas bara la Ulaya zimeanza kuonyesha matunda yake ambapo staa huyu ametua huko Ujerumani na kufanya onyesho Berlin.

msanii wa hip hop nchini Kenya Octopizzo

Octopizzo amefanya onyesho hili katika tamasha kubwa kabisa la Hip Hop la Rap Am MIttwoch ambalo ni kubwa kabisa huko Berlin, na kufungua milango mingine mikubwa zaidi ya michongo ya kimataifa katika sanaa ya rapa huyu.

Octopizzo kwa sasa anafanya vizuri katika chati na kazi inayokwenda kwa jina Something for You ambayo inaendelea kupokelewa sawa sawa katika kipindi kifupi tu tokea kuachiwa kwake.