Tuesday , 4th Aug , 2015

Super Nyamwela, msanii wa muziki na msakata dansi mkongwe hapa nchini, ameweka wazi mpango wake wa kurasimisha namna ya kusaidia kukuza vipaji vya kudansi hapa nchini.

msanii wa muziki na msakata dansi mkongwe nchini Tanzania Super Nyamwela

Nyamwela amesema kuwa lengo ni kuanzisha taasisi ambayo itatoa mafunzo na vyeti kwa wahitimu wa fani hiyo muhimu kwa upande wa burudani.

Nyamwela ameiambia eNewz kuwa, yupo katika mpango wa kukamilisha vibali vya taasisi hiyo, ambayo itajikita katika kufunza dansi za kitamaduni kutoka maeneo mbalimbali nchini, lengo likiwa ni kubadili pia mtazamo na kuijengea heshima fani ya kudansi na wahusika wake.