Monday , 5th May , 2014

Msanii wa muziki wa Genge kutoka nchini Kenya, Nonini pamoja na marafiki zake wameibuka na njia mpya ya kuchangisha pesa kwaajili ya shughuli za hisani, na hii ni kupitia mashindano ya wa mpira wa kikapu ambao huzikutanisha timu mbali.

Mashindano haya ya mpira wa kikapu yamepatiwa jina (Entertainment With Fun 4 Charity), ambapo kwa mujibu wa Nonini, yatakuwa yakifanyika kila sikukuu, huku wakiwa wamepanga kukutana tarehe 1 mwezi June tena kwaajili ya mechi nyingine kali.

Katika mashindano ya kwanza yaliyofanyika, kiasi cha shilingi za Kenya 120000 zilipatikana, ambapo asilimia 50 ya pesa hizi ilipelekwa katika kituo cha kulelea watoto cha Filomena kilichopo huko Kayole.

Tags: