Tuesday , 4th Mar , 2014

Rapa Nonini kutoka nchini Kenya, ambaye kwa muda sasa amekuwa akijishughulisha katika kuwasaidia kwa namna mbali mbali watu wenye ulemavu wa ngozi, sasa ameamua kutanua zaidi wigo wa msaada wake ambapo amefanikiwa kufika huko Wajir na kutoa misaada mbalimbali kwa watu wenye albinism.

Nonini kupitia taasisi yake ya Colour Kwa Face amefikisha msaada wa lotion za kujikinga na
mwanga wa jua ambao huwaathiri kwa kiasi kikubwa walemavu hawa wa ngozi, ambapo kupitia ukurasa wake wa facebook ameweka picha kadhaa kuonyesha namna misaada hii ilivyowafikia walengwa.

Hii imekuwa ni moja ya mambo makubwa ambayo Nonini amekuwa akiyafanya kando ya muziki kama jitihada za kurudisha shukrani kwa jamii kwa mafanikio yake kimuziki, jambo ambalo ni mfano mzuri wa kuigwa na wasanii pamoja na jamiii kwa ujumla.