
Tunda Man
Akiongea ndani ya eNewz Tunda amewapongeza wasanii wezake waliofunga ndoa akiwemo Nyandu Tozi, Mwana Fa , Mabeste na wengine Tunda amewasihi wasanii wenzie wa dini ya kiislamu kufunga ndoa kwa kuwa zitawasaidia kuongeza heshima katika jamii inayowazunguka.
Hata hivyo Tunda amewachana wasanii wanaoongopa kufunga ndoa wakihofia kushuka kwa muziki wao kwamba hawana hofu ya Mungu kwani kupanda na kushuka ni mipango ya Mungu na wapo kina Mr. Blue wamefunga ndoa na bado wanafanya vizuri kimuziki.