Wednesday , 14th Dec , 2016

Msanii wa bongo fleva Alikiba aliyeshinda tuzo tatu usiku wa EATV AWARD ikiwemo video bora ya mwaka, mwanamuziki bora wa mwaka na wimbo bora wa mwaka  ameshukuru kukutana na Dully na kusema hana tatizo nae na kwamba anampenda sana.

Dully Sykes (Katikati) akiwa na Alikiba (Kulia) wakifanyiwa mahojiano na Duwe wa eNewz

 

Akiongea ndani ya eNewz wakati wa tuzo hizo Kiba amesema "Dully ndyo sababu ya mimi kuwa Kiba kwani kila nilichokuwa nakiimba Dully alinisapoti na wakati mwingine  kilikuwa kinamtoa machozi na nisipofika kwa kina Dully alikuwa ananitafuta mpaka anipate na ukizingatia sikuwa na simu nitampenda Dully mpaka kufa kwangu" alisema Kiba.

Pia Dully hakusita kumuombea Kiba afike mbali na kupata mafanikio ili kufikisha muziki wetu mbali na amesema mambo yakiwa sawa mwakani atakuwa mmoja kati ya washiriki wa EATV AWARD na kusisitiza kwamba hana tatizo na Kiba.

Tazama hapa:- 

Tags: