Saturday , 18th Apr , 2015

Rapa Nikki Mbishi, ambaye kwa kushirikiana na One The Incredible pamoja na Chidi Beenz wameachia rekodi mpya inayokwenda kwa jina Yeeah, ametoa wito kwa mashabiki, kusapoti zaidi kazi za wasanii na mambo hasi wanayofanya ili kuwasaidia kufika mbali.

Nikki Mbishi, Chidi Beenz na Invincible_Ktb

Nikki Mbishi amesema hayo akigusia suala zima la Chidi Beenz ambaye hivi karibuni amevuka kiunzi cha misukosuko na vyombo vya dola, ikiwa ni upande wa maisha yake nje ya muziki, wakiwa sasa wameunganisha naye nguvu kurudi tena katika chati kisanaa.

Kutazama hili na mahojiano yao kwa undani zaidi, Tafadhali usikose kutazama Planet Bongo kupitia EATV, Jumatatu hii saa 3 kamili usiku.

Timu hii ya watu watatu ikiwa na ukaribu mkubwa sana kwa sasa sambamba na rekodi kadhaa kwa pamoja, Nikki amesema, ni vizuri kumulika zaidi maisha ya kikazi ya msanii, kuliko yake ya binafsi ili kumsaidia kukua.