Soggy Doggy akiwa katika Planet Bongo iliyokuwa ikiruka mubashara kutoka Mabibo, Jijini Dar es Salaam
Soggy Doggy alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho leo kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutoka Mabibo Mwisho Jijini Dar es Salaam, Soggy anasema kwa wasanii wa hip hop sasa akimsikiliza rapa Country Boy ni kama anamsikiliza marehemu Albert Mangwea.
" Vijana saizi wanafanya poa sana ndiyo maana na mimi nataka niende nao sawa, sitaachia kazi mpya sasa mpaka nione nimekamilisha video kali kabisa ila kazi zipo nyingi sana ndani, ila kuna huyu mtoto Country Boy napomsikia kazi zake ni kama namsikiliza Albert Mangwea" alisema Soggy Doggy



