Monday , 4th Aug , 2014

Aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo nchini Kenya Derrick Amuga ambaye alijijengea jina kupitia tamthilia maarufu ya Tausi katika miaka ya 90 akitambulika kama Master Sugu, amefariki dunia.

Muigizaji Derrick Amuga wa nchini Kenya

Taarifa za msanii huyu kufariki zimekuja baada ya kupotea kwa siku kadhaa akiwa anatafutwa na jamaa zake tangu Julai 25, na baadaye mwili wake kupatikana katika Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, na kwa sasa uchunguzi wa chanzo cha kifo chake unafanyika.

Msanii huyu alipotea katika sanaa ya uigizaji kwa muda baada ya kurejea nyumbani kwao huko Kakamega kujipanga zaidi kisanii, kabla ya kurejea tena Nairobi hivi karibuni kuendelea na kazi hiyo.