Tuesday , 22nd Jul , 2014

Msanii Delvin Mudigi kutoka kundi la Sauti Sol ameonesha upande mwingine wa kipaji chake katika tasnia ya burudani, na hii ni kwa upande wa uigizaji kupitia ushiriki wake katika tamthilia maarufu inayokwenda kwa jina Veve ya huko Kenya.

Msanii wa muziki Delvin Mudigi nchini Kenya

Tamthilia hii ambayo Delvin anazidi kung'arisha nyota yake kwa kushiriki ndani yake, inatarajia kufanya vizuri hasa kutokana na timu yake ya utayarishaji kujipanga na kukamilika, ikishirikisha watayarishaji wa filamu maarufu ya Nairobi Half Life na watayarishaji filamu makini kutoka Ujerumani.

Ndani ya filamu hii Delvin anafahamika kama Veve na kutokana na kujijengea umati mkubwa wa mashabiki kupitia muziki, tayari amekuwa kivutio kikubwa katika kazi hii mpya.