
Floyd Mayweather na Manny Pacquiao
Majibu ya Cyrill Kamikaze baada ya kuulizwa ni nani anaweza kushinda mpambano huo, ni kuwa kila mmoja anaweza kuchukua ushindi endapo atakuwa makini na kusoma game ya mwenzake, ambapo kwa ufafanuzi zaidi, unaweza kutazama alichokisema kupitia link hii https://www.youtube.com/watch?v=R3F4i74Bol0
Prince Dully Sykes kwa upande wake, ameweka wazi kuwa ni Team Pacquiao, itokee bondia huyo ameshinda ama ameshindwa, huku akiweka wazi kuwa havutiwi na maneno mengi na mbwembwe za Mayweather.
Hayo ni baadhi tu ya maoni ya mastaa wetu, unafikiri ni nani atashinda mpambano huu, tafadhari weka maoni yako hapo chini.

