Thursday , 23rd Jun , 2016

Msanii Linex Sunda Mjeda, amefunguka hisia zake juu ya watu hususan vijana na wasanii wanaotumia madawa ya kulevya, bila kujali madhara yake.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Linex amesema watu hao wanatakiwa watambue kuwa wanapotumia madawa ya kulevya, sio tu wanajiharibia maishayao, bali pia wanawaumiza wazazi wao, ambao wamewahangaikia kuwalea.

"Unapiga piga debe ili upate hela ya kwenda kuvuta unga, mama yako akikuona pale akiwa anapita tu amepanda daladala akiukona pale, imagine atajisikiaje, lazima hivyo vitu vijana waimagine pia, wajue kwamba sawa huwa wanaharibikiwa maisha yo binafsi, lakini pia huwa wanawatoa machozi wazazi wao au familia zao", alisema Linex.

Linex aliendelea kusema....."Kwa hiyo tusizungumzie tu wasanii ambao wanatumia dawa hizo za kulevya, tuizungumzie jamii na vijana wenzetu amabo wanatumia madawa ya kulevya, wajue kwamba wanapoharibikiwa baada ya kujiingiza kwenye madawa ya kulevya, wanawaumiza watu wengi, wanapowaona wamshaharibikiwa".

Pia Linez amesema watu hao wasisubiri mpaka familia zao kuwakamata na kuwapeleka rehab, bali wenyewe wajiongeze na kwenda ili kupata tiba ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.