
Yusuph Mlela
Yusuph Mlela amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya taarifa zilizokuwa zinaendelea kwamba wamegombana sababu ya mwanamke.
"Hemed ni rafiki yangu sijawahi kugombana naye kabisa, hizo zilikuwa ni stori tu, hayo ni mambo tu yalitokea watu hawajui kiundani, ilikuwa ni kutoelewana kwa kawaida ila sasa hivi tupo vizuri, tunafanya kazi pamoja".
Aidha msanii huyo amesema anapenda sana nywele zake kuliko kitu chochote, tangia ameanza kujitambua akiwa ana umri wa miaka 17 au 18 alikuwa anafuga nywele kwa mtindo wa Afro, kusuka au anaziachia anavyototaka.