Wednesday , 7th Sep , 2016

Msanii Mr Blue amedai kuwa watu wengi walikuwa wakitamani kuona 'collabo' kati yake pamoja na Alikiba jambo ambalo lilikuwa linawindwa kwa muda mrefu na kusema kuwa watu wengi walikuwa wakimshauri afanye kazi na Alikiba

Mr Blue (kushoto0 katika video ya 'mboga saba'

Mr Blue amesema hayo kupitia kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kwamba watu wengi walikuwa wakimshauri yeye afanye kazi na Alikiba pia Alikiba alikuwa anashauriwa na watu pia afanye kazi na Mr Blue.

"Ushirikiano wa kazi yangu mimi na Alikiba ulikuwa unawindwa kwa muda mrefu sana, watu wengi walikuwa wanaomba mimi nifanye kazi na Alikiba na Alikiba walikuwa wakimwambia kama utafanya kazi na Mr Blue itakuwa kitu kizuri kwa sababu ni ndugu na mmetoka sehemu moja, mmeshirikiana katika mambo mengi nje ya muziki, nashukuru Mungu kitu hicho kilifanyika na matokeo yake yameoneka kwani mbali na kupata pesa ambazo nimeingiza kwa muda mfupi toka wimbo kutoka lakini wimbo wangu umebahatika kuchezwa katika kituo kikubwa Afrika bila mimi kupeleka kazi hiyo" alisema Mr Blue

Mbali na hilo Mr Blue amedai kuwa mafanikio mengine katika wimbo huo ni pamoja na kuwa na 'viewers' zaidi ya milioni moja 'Youtube' hivyo imekuwa ni video ya kwanza ya Hip hop kutoka Tanzania kufikisha watazamaji wengi 'Youtube'