Saturday , 25th Jul , 2015

Star wa muziki Marlaw, amemtaja nyota mkongwe wa muziki wa R&B kutoka Marekani, kuwa ndiye msanii ambaye alimvutia na kumhamasisha binafsi kuona ndoto yake ya kuwa mwanamuziki inawezekana, mpaka kuchukua hatua ya kuanza kuimba na kufikia alipo sasa.

Pipi akiwa na Marlow

Kama sehemu pia ya kuhamasisha vijana wengine kufuata ndoto zao, Marlaw amesema kuwa rekodi za R Kelly kwa kiasi kikubwa zimekuwa kama mafuta ya safari yake kimuziki, star ambaye amewezesha kipaji chake kikakua na kutengeneza rekodi kali kabisa katika historia ya muziki wa Bongo Flava.