Monday , 14th Jul , 2014

Baada ya kupotea gizani huku wasanii wakijiuliza maswali mengi, hatimaye msanii Kenzo aibuka na ujio mpya katika gemu.

Msanii wa nchini Kenya Kenzo

Akiwa anatamba na wimbo wake 'Kidogo Tu' mkali huyo wa nchini Kenya amesema kuwa hivi sasa anajiandaa kufyatua single yake mpya aliyoibatiza jina 'Mama' ukiwa ni wimbo ambao ni mahususi kwa ajili ya kumbukumbu ya marehemu mama yake.

Wimbo huo ambao umetayarishwa na Maich Blaq utakuwa ni wimbo wake wa kwanza baada ya kuachana na labo ya Ogopa Djs.