Friday , 2nd Jan , 2015

Msanii wa muziki Madee, a.k.a Rais wa Manzese, amekuwa ni moja kati ya wasanii wa kwanza kabisa kuzungumzia mwaka 2015 kisiasa, ambapo msanii huyu amesema kuwa utulivu ndio kitu cha muhimu anachopenda kushuhudia kwa watanzania.

msanii wa muziki wa bongofleva Madee

Madee amezungumzia haya haswa katika kipindi hiki kwa watanzania kwa mwaka huu kuelekea katika uchaguzi.

Madee amesema haya akitolea mfano wa kuwepo kwa misuko suko katika matukio kama haya kwa nchi nyingine, na kusisitiza kuwa angependa kuona Rais ajaye anapatikana kwa amani na utulivu na hapa anazungumza zaidi.