Monday , 22nd Jun , 2015

Nyota wa muziki Madee, ameeleza kuwa anajivunia kolabo yake ya gemu ilivyochange aliyofanya na msanii wa muziki Godzilla, ndiyo rekodi ambayo imefungua mtindo wa muziki wa majadiliano katika gemu ya Bongofleva.

Madee amesema kuwa, rekodi hiyo ilifanyika kutokana na hali halisi na mabadiliko katika muziki kwa kipindi ambacho ilirekodiwa, na alifanya na Godzilla akiwa kama msanii aliye juu kwa kipindi hicho na hivyo kuzaliwa kwa mfumo huo mpya kabisa wa kolabo katika Bongo Flava.