Saturday , 24th Jan , 2015

Star wa muziki Mabeste, ambaye ametoka na rekodi yake mpya ya kufungulia mwaka inayokwenda kwa jina 'Usiwe Bubu', ameeleza kuwa, nafasi ya mkewe kama meneja imesaidia kwa kiasi kikubwa kumjenga.

Lisa, Mabeste na Kendrick

Mabeste amesema kuwa fursa hiyo imepanua zaidi wigo wa sanaa yake ya muziki, mwaka huu wakiwa na mipango mingi inayolenga kusaidia kuinua vipaji vya vijana.

Mabeste a.k.a Baba Kendrick amesema kuwa, katika kipindi cha nyuma, Sanaa yake ilikuwa zaidi ni juu ya Studio, Interviews na Show lakini sasa chini ya uongozi wa Mama Kendrick imekuwa ni zaidi ya hapo, wakijiongeza zaidi katika kufikia vipaji katika jamii na kuviinua.

Mabeste amesema kuwa mpango huu utahusisha michezo ya riadha na pia kuzunguka katika mashule mbalimbali kutafuta wanafunzi wenye uwezo kisanaa na kujaribu kuweka njia bora ya kuviendeleza kwa kushirikiana na walimu na wazazi wao.