Saturday , 5th Nov , 2016

Star wa ngoma ya 'BAADAE SANA' anayekwenda kwa jina la Mabeste, amefunguka na kuwaponda wasanii wanaotegemea kuuza kazi zao kupitia skendo za kutengeza ili kutafuta kiki.

Mabeste na Mkewe wakiwa ndani ya FNL ya EATV

 

Mabeste ambaye hivi karibuni amefunga ndoa ya kimyakimya na mpenzi wake Lissa, ametoa kauli hiyo akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV, ambapo alisema anakerwa na wasanii wenye tabia ya kufanya mambo yasiyo ya kimaadili ili kuzusha skendo kwa madai ya skendo hizo kuwasaidia kimuziki na kupaisha majina yao.

Aliulizwa kuwa haoni kwamba uamuzi wake wa kuamua kufunga ndoa utamfanya asiwe na skendo ambazo mara nyingi huwakumba wasanii ambao hawajaoa, jambo linaloweza kumuondoa kwenye game?

Mabeste alijibu kuwa haoni umuhimu wa skendo kama haziijengi jamii, na kusisitiza kuwa kwake jambol la muhimu ni lile lenye mafundisho kwa jamii na kwamba kama skendo hizo hazina mafunzo kwa jamii kwake hazina faida.

"Kuingia kwenye ndoa hakuwezi kunifanya nikapotea kwenye muziki, kama ni skendo haziwezi kumtoa mtu na wala siyo njia njia nzuri ya kutoka, kama unahitaji kiki basi tengeneza kiki ambazo zitamfanya mtu kujifunza kitu, siyo kiki ambazo hazina mafunzo" Alisema Mabeste.