Thursday , 13th Mar , 2014

Rapa M Rap, baada ya kutoka kwa misukosuko chini ya lebo ya B Hitz hivi karibuni, ametangaza ujio wake mpya kutoka AM Records, kwa kuja na traki yake mpya inayokwenda kwa jina “Usiende Mbali” ambayo ndani yake amemshirikisha na msanii Jux Vuitton.

M Rap amesema kuwa kazi hii mpya inabeba ujumbe wa mapenzi kwa ajili ya kuwapa moyo wapendanao ili kudumisha zaidi mahusiano yao, na kusema kuwa kazi hii mpya ndio mwanzo wa kufungua vyema mwaka huu wa 2014.

Aidha rapa huyu amewaomba mashabiki na wadau wote kuumpa sapoti kwani kazi zingine mpya zinatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka huu.