Saturday , 22nd Nov , 2014

Mkurugenzi wa Lino Agency, Kampuni yenye dhamana ya kuendesha mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amesema kuwa hakuna mpango wowote wa kurekebisha kanuni na taratibu za kuwapata washiriki wa mashindano hayo ya urembo, licha ya kuonekana

Kuwepo kwa udanganyifu na hujuma kwa washiriki ambao huwania taji hilo.

Hashim bila kupindisha maneno amesema kuwa, Marekebisho ya kanuni na vigezo vya kuwapata washiriki kutaleta athari kubwa hasa katika kubana uhuru wa warembo katika mashindano.

VIlevile Hashim akazungumzia Mashindano ya Miss World ambayo yatafanyika mwezi ujao, Tanzania ikiwa inawakilishwa na mrembo Happyness Watimanywa, ambapo sambamba na baraka zake, amesema kuwa Mrembo Happy atatumia nafasi hii kuitangaza vizuri Tanzania, na katika mashindano haya magumu, ana nafasi sawa sawa na washiriki wengine kushinda taji hilo.