Tuesday , 25th Nov , 2014

Msanii wa muziki wa Bongofleva, Leah Muddy amezungumzia hatua yake ya kuamua kuigeukia imani na kufanya muziki wa ujumbe wa Mungu, sababu yake ikiwa ni maisha yake ya awali kutokumpatia amani ya moyo.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Leah Moudy

Leah amesema kuwa, baada ya kutafakari sana ameamua kumgeukia Mungu, na kuingia katika maisha ambayo anaona anapata amani, hatua ambayo imebadilisha hata aina ya muziki anaoufanya na kuhakikisha kuwa rekodi zake zinakuwa zinabeba ujumbe wa kiimani zaidi.