Saturday , 10th Dec , 2016

Msanii mahiri wa vichekesho kutoka kundi la Ze Comedy la EATV, Mtanga ameudhihirishia ulimwengu kuwa naye ni mahiri katika masuala ya mavazi na muonekano baada ya kuongoza moja ya Red-Carpet katika Tuzo za EATV.

Mtanga katika Red Carpet

Mtanga ambaye ameshirikiana vizuri na warembo pia kutoka EATV, Vannila na Suzie, ameweza kuonesha kuwa uwezo wake si kuchekesha pekee, bali pia katika masuala ya muonekano pia anatisha.

Ameweza kuongoza mapokezi ya mastaa kibao na kufanya mahojiano kuhusiana na viwalo vyao.

Mwenyewe anasema suala la viwalo kwake ni sehemu ya maisha kwa kuwa huwezi kuwa msanii bila kuwa mchambuzi wa viwalo.

Vanila

 

Tags: