Rapa mkali kutoka Afrika Kusini, K.O.
Kupitia njia ya kurasa zake za mitandao ya kijamii, K.O ameweka ujumbe kwa mashabiki wake katika maeneo hayo kuthibitisha juu ya ujio wake huo, ambapo atapata fursa ya kutembelea vituo mbalimbali ikiwepo Ting'a Kali Namba Moja kwa Vijana (EATV).
Hii inakuwa ni nafasi kwa mashabiki wa msanii huyo kutoka eneo hilo la Afrika kumfahamu kumsikia na kumuona kwa karibu, akifahamika sana kwa kolabo ya 'Nobody But You' aliyofanya na Vanessa Mdee, sambamba na rekodi zake kali kama 'Cara Cara' na 'Son of a Gun'.