Josh Muruga na Salama Jabir
Tuzo hii ilipokelewa na timu nzima ya Mkasi ikiongozwa na mtangazaji wake mahiri, Salama Jabir ambaye ametoa shukrani kwa Watu walioonyesha mapenzi na kipindi cha Mkasi mpaka kukiwezesha kushinda.
Tuzo hizi zilizokuwa na vipengele 11 tofauti, pia zimehusisha Vipindi Bomba na Makini vya EATV na East Africa Radio, kama vile Planet Bongo na Friday Night Live, Vilevile Mtangazaji Sam Misago na Salama Jabir katika orodha ya waliokuwa wanawania tuzo.
Tuzo hizi zimeandaliwa na mtandao wa habari za Burudani Tanzania na kufanyika zikiambatana na burudani mbalimbali za muziki na vichekesho.