Friday , 23rd Oct , 2015

King Dee msanii toka Kenya anayekuja vizuri katika gemu, amesema kuwa amejipanga vizuri sana katika kufanya muziki mzuri ili aweze kuiwakilisha vizuri Afrika Mashariki kupitia muziki wake anaofanya.

King Dee ambaye anatamba na nyimbo mbili zilizovuma sana zijulikanazo kwa jina la 'Siko kamili' na ' Nipe Tamu' anaamini kuwa katika wasanii wanaotarajiwa kuwa wakubwa Afrika Mashariki yeye ni miongoni mwao maana anasema ana kipaji kikubwa na anajua kufanya muziki mzuri.

" Napenda watu wafahamu kwamba nimejipanga kufanya muziki mzuri na wataupenda sana, hata kama mtu aliyesikiliza nyimbo zangu za Nipe utamu na siko kamili ataelewa kitu gani namaanisha, nimejipanga kuiletea Afrika Mashariki tuzo nyingi sana za ndani na nje maana ninajiamini ninaweza kufanya hilo kupitia muziki wangu" alisema King Dee

King Dee ameomba watu kutoka nchi za Afrika Mashariki na nje waweze kumpa sapoti kubwa maana anaamini hatowaangusha na anamini sapoti yao ndio itafanya yeye aweze kufika mbali zaidi

Unaweza kubofya hapa kuusikiliza wimbo wake huu wa Nipe tam https://www.youtube.com/watch?v=eAxW_VZRTuM&feature=youtu.be