Saturday , 14th Jun , 2014

Wakazi wa Mji wa Songea na vitongoji vyake sasa ni wakati wao wa kuonja burudani ya ukweli na ya uhakika ya Kilimanjaro Music Tour, ambayo itadondoshwa pale katika uwanja wa Uwanja wa Majimaji na wasanii wakali wanaokubalika hivi sasa hapa Tanzania.

Kili Music Tour 2014

Mpango mzima utafanyika kesho Jumapili ya tarehe 15 kuanzia saa nane mchana, ambapo jukwaani sasa watapanda nyota hapa Bongo, akiwemo Diamond Platnumz, Shilole, Ommy Dimpoz, Weusi, Linex, Khadija Khopa, Mwasiti, Ben Pol na Professor J.

Shughuli nzima inaongozwa jukwaani na timu ya East Africa Radio na East Africa Television, ambapo katika mstari wa mbele akisimama Zembwela, vilevile mjukuu wa Ambua aka Dullah pamoja na mkali mwenyewe Dj Summer!.

Na ili kuzungusha Kikwetu Kwetu kwa shangwe utalipa kiingilio cha shilingi 2,500 mlangoni na kupatiwa kinywaji chako cha bure pia vyakula vya kutosha vitakuwepo. Kili Music Tour 2014 ni Kuzungusha Kikwetu Kwetu!