Monday , 3rd Nov , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Kenzo amejipatia kazi mpya kama wakala wa kusimamia haki za Chama cha Watumbuizaji cha Kenya pamoja na Umoja wa Watayarishaji Muziki wa nchi hiyo.

msanii wa muziki nchini Kenya Kenzo

Vyama hivi viwili wimeundwa kwa hazi ya kukusanya haki za mirahaba/royalties za Watayarishaji muziki na watumbuizaji, kwa maana ya wasanii kwa mujibu wa Kenzo mwenyewe.

Msanii huyu amwewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, nafasi hii mpya haitaingiliana kwa namna yoyote na muziki wake, na itakuwa kama nafasi ya kumkutanisha na wadau wengi zaidi ambapo pia wanaweza kusaidia kusogeza muziki wake mbele.