Monday , 30th Nov , 2015

Star wa muziki kutoka Kenya, Juliani amejikita katika jitihada za kuchanga pesa kusaidia gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa wa kiarusi yanayomkabili mwandishi mahiri Binyavanga Wainaina.

Staa wa muziki kutoka Kenya, Juliani

Juliani ameeleza kuwa hii ni sehemu ya kurejesha fadhila kwa msaada mkubwa wa mwandishi huyo katika sanaa yake na imani ambayo mtu huyu aliijenga kwake na kundi zima la Ukoo Flani Mau Mau, uwekezaji na hamasa ambayo amewapatia ndio iliyowasaidia kusonga mbele mpaka kufikia mafanikio wanayojivunia sasa.

Kwa kuonesha kuguswa na kuwa ni sehemu ya suala hilo, Juliani ametumia majukwaa mbalimbali ikiwepo mitandao ya kijamii kuwafikia wasamaria wema, wakiwa na lengo la kukusanya zaidi ya shilingi milioni 7 za Kenya kumtibu Wainaina.