Joel Lwaga
Akizungumza kwenye Weekend Breakfast ya East Africa Radio, Joel amesema alipokuwa akisoma sekondari kidato cha tano, alipata matatizo ya moyo yaliyompelekea kupooza, hali ambayo ilimkatisha tamaa na kumrudisha nyuma kwa mwaka mmoja, lakini alipona kwa miujiza ya Mungu.
“Nilipokuwa kidato cha tano, nilipooza nikawa mtu ambaye siwezi kufanya chochote, ilikata tamaa, nilihisi ni mtu ambaye nakufa, nikakaa nyumbani takriban mwaka mzima, nilipokaribia kufanya mtihani wa kidato cha sita nikapona tu kimiujiza", amesema.
"Baba alikuwa anasikitika nitafanyaje mtihani, kwa sababu nilikuwa nasoma shule za serikali, na wenzangu walishanijazia kila kitu nikakataliwa kurudia mwaka, nikamwambia tu baba, mimi nitakwenda kufanya mtihani, siku ya pili nikanyanyuka ikawa ni miujiza, kila mtu alinishangaa, nilikuwa nishaombewa huko nyuma lakini muujiza ukawa bado haujatokea, mpaka daktari aliyekuwa akinifanyia vipimo akashtuka”, ameogeza.
Joel Lwaga ambaye sasa anatamba na wimbo wake wa 'sitabaki kama nilivyo', pia amesema kwamba ugonjwa huo ulitokana na tatizo kwenye valve za moyo wake, lakini sasa hivi kwa maombi aliyoyapata limeisha na hafungi tena safari za kwenda kumuona daktari.



