Wednesday , 18th Feb , 2015

Rapa Dogo Janja ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa katika gemu ya muziki hapa Bongo, anatarajiwa kurejea kwa kishindo April 23, siku ambayo pia ndio itakuwa ni siku ya kuzaliwa msimamizi wa kazi zake, Rapa Madee.

Madee na Dogo Janja

Ujio huu mpya wa Dogo Janja unakuwa ni zawadi kutoka kwa staa huyo, na rekodi ambayo ataachia itakuwa ni kolabo ambayo amefanya na Jux, na hapa Madee anaeleza zaidi juu ya mpango huo.