Tuesday , 21st Jun , 2016

Meneja wa rapper Young Dee anayejulikana kwa jina la Maximillian, amesema hivi karibuni watu watajua mbivu na mbichi kuhusu msanii huyo, ambaye alikuwa anamsimamia na kuamua kuachana naye.

Akiongea kwenye Planet Bongo, Maximillian amesema kuna mambo mengi yametokea baada ya yeye na Young Dee kuacha kufanya kazi pamoja, lakini baada ya kurudi anakusudia kuweka wazi mamabo mbali mbali kuhusu msanii huyo, ambaye hivi karibuni alikumbwa na kashfa ya kutumia madawa ya kulevya.

"Itakuwa ni kuhsu mambo mengi ambayo yalizungumzwa kuhusu Young Dee, ukweli kuhusu Young Daresalama, nafikiri ndio kitu cha msingi kwa sababu waandishi wa habari ana maswali kwa Young Dee, kwa hiyo tumemaua kutengeneza platform ya kuyajibu maswali yote", alisema Maximillian.

Hivi karibuni Young Dee alionekana tena akiwa na meneja wake huyo ambaye aliacha kufanya naye kazi, kitendo ambacho wadau wengi wa muziki walimlaumu rapper huyo, huku sasa hivi kukiibuka taswira ya kuwa na matumaini ya wawili hao kufanya kazi tena.