Sunday , 16th Mar , 2014

Tamasha la filamu linalokuwa kwa kasi sasa nchini Rwanda lijulikanalo kama 'Hillywood' limeandaa maonyesho kwa ajili ya kumubukumbu ya miaka ishirini ya mauaji ya halaiki yaliyotokea mweka 1994 nchini humo.

Tamasha hilo litakalofanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Julai 12 limepewa jina la 'Reflection' na litajumuisha filamu za ndani na nje ya nchi haswa zile zinazoangalia historia inayohusu Afrika na dunia kwa jumla hususan nchi ya Rwanda.

Katika tamasha hilo waandaaji pia wamepanga kuwatambua na kutoa heshima kwa waandaaji wa filamu nchini Rwanda ambapo mshindi atapata jumla ya dola 250 na tiketi ya kwenda popote anapotaka kupitia maeneo ambayo shirika la ndege la uturuki linapofika.

Tamasha hilo lilianzishwa mwaka 2005 na limeendelea kukua kwa kasi ambapo hivi sasa limekuwa kama sehemu ya utamaduni wa Rwanda.