Wednesday , 29th Oct , 2014

Wasakata Dansi mahiri wakishirikiana timu ya East Africa Television, Ting'a Namba Moja kwa vijana, leo hii wamekuwa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuonyesha burudani kwa wapenzi wa kituo hiki mahiri.

Timu ya EATV na Madansa Mitaani leo

Tukio hili ambalo limekuwa kivutio kikubwa, limedhihirisha uwezo mkubwa wa kituo hiki katika kutoa burudani na vilevile kuisogeza karibu kabisa na wapenzi wake kwa kujumuika nao mitaani kwao katika mishemishe zao za kila siku za kuendesha maisha.