Friday , 7th Oct , 2016

Msanii Diamond amesema ana imani EATV AWARDS kuwa zitakuwa zenye ubora, kwani EATV LTD imekuwa na mazoea ya kufanya vitu vyenye ubora miaka yote.

Diamond Platnumz akiwa kwenye FNL leo Oktoba 7, 2016

Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Diamond amesema anasikitishwa pale anapoona tuzo zinakuwa na jina kubwa lakini kwenye tuzo yenyewe inakuwa haina ubora unaofanana na thamani yake.

“Natumai East Africa wamefanya suala la enterinment kwa miaka mingi tena kwa quality nzuri, studio nzuri, vifaa vizuri, tunategemea pia kwenye tuzo zitakuwa zina quality, unajua tuzo ile 'trophy' unayobeba nyumbani ndiyo tuzo yenyewe, sasa unakuta tuzo nyingine zina jina kubwa lakini tuzo yenyewe haina ubora, kwa hiyo natumai watatoa kitu chenye quality”, alisema Diamond'

Pia Diamond amesema ana imani tuzo hizo zitasaidia kuinua tasnia ya filamu kwani kwa muda mrefu filamu za Tanzania zimekuwa zikikosa changamoto ya kuiinua.

“Kwa muda mrefu filamu zetu wanajitahidi kufanya kazi lakini zinakosa kupiga hatua kwa sababu hakuna kitu kinachoipa changamoto, zikipatikana tuzo zinazoipa changamoto itasaidia kuinua kwa sababu pia ni heshima”, alisema Diamond.

Pia Diamond amsema ana imani tuzo hizo zitatolewa kwa haki bila upendeleo kwa msanii, kwa sababu moja au nyingine.

Tags: